Exodus 29:1-6

Kuweka Wakfu Makuhani

(Walawi 8:1-36)

1 a“Hili ndilo utakalofanya ili kuwaweka wakfu makuhani ili wanitumikie mimi katika kazi ya ukuhani: Chukua fahali mchanga mmoja na kondoo dume wawili wasio na dosari. 2 bKutokana na unga laini wa ngano usiotiwa chachu, tengeneza mikate na maandazi yaliyokandwa kwa mafuta, pamoja na mikate midogo myembamba. 3Viwekwe vyote ndani ya kikapu na kuvitoa pamoja na yule fahali na wale kondoo dume wawili. 4 cKisha mlete Haruni na wanawe kwenye lango la Hema la Kukutania na uwaoshe kwa maji. 5 dChukua yale mavazi na umvike Haruni koti, joho la kisibau na kisibau chenyewe pamoja na kile kifuko cha kifuani. Mfungie hicho kisibau kwa ule mshipi wa kiunoni uliosukwa kwa ustadi. 6 eWeka kilemba kichwani mwake na kuweka taji takatifu ishikamane na hicho kilemba.
Copyright information for SwhKC